MAANA YA EBOLA:
Ebola ni ugonjwa hatari sana wa mlipuko unaosababisha kifo kwa waathirika kwa wepesi sana. Ugonjwa huu huwapata binadamu na wanyama wa mwituni( hayawani) kama vile kima, sokwe, popo, ndege, mijisi, afibia, nk. Ebola husababishwa na virusi viitwavyo “Ebola Virus” kwa Kingereza.
Licha ya ukweli kwamba Virusi vya Ebola havipatikani sehemu maalumu, wataalamu wanasema kuwa virusi hivyo vinapatikana zaidi barani Afrika kutokana na ukweli kwamba mnyama mwenye virusi hivyo anapatikana zaidi barani Afrika.
Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola umetokea katika nchi nyingi za Afrika mpaka sana na hivyo kuuwa watu wengi sana, na bado unaendelea kupukutisha maisha ya watu wengi mpaka sasa. Ugonjwa huo umelipuka na kuathiri zaidi watu wa nchi kama Liberia, Sierra Leone, Guinea, Ghana, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Gabon, Sudan, Ivory Coast, Uganda, nk. Ugonjwa huu ambao unaendelea mpaka sasa, umeuwa maelfu ya watu wakiwemo wauguzi wa waathirika.
NAMNA UNAVYOAMBUKIZWA:
1. Kugusana moja kwa moja na mtu ama mnyama mwenye ugonjwa huo,
2. Kugusana moja kwa moja na damu ama majimaji (mate au mafua) ya mtu mwenye ugonjwa huo
3. Kugusa vifaa vya tiba vilivyo na virusi vya ugonjwa huo kama sindano;
4. Kutumia vifaa visivyochemshwa katika hospitali kama sinano,
5. Kushika au kugusa kinyesi cha mnyama mwenye ugonjwa huo,
6. Kuvuta hewa yenye virusi vya ugonjwa huo, hasa katika mazingira ya hospitali yenye waathirika wa Ebola.
7. Kutumia nyama ya wanyama walioathirika kama kitoweo na
8. Kutozingatia tahadhari za kitaalam.
DALILI ZA EBOLA:
Mtu au mnyama mpaka aonyeshe dalili za ugonjwa wa Ebola huchukua kati ya siku 2 hadi 21. Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na:
1. Homa kali,
2. Kuumwa kichwa,
3. Kuharisha,
4. Kutapika,
5. Maumivu ya kifua,
6. Maumivu ya tumbo,
7. Mafua,
8. Kikohozi,
9. Maumivu ya misuli na viungo (joints),
10. Kuvimba koo,
11. Mwili kuwa dhaifu,
12. Mfadhaiko,
13. Kuchanganyikiwa,
14. Macho kuwa mekundu,
15. Kuvuja damu kwa ndani na nje, nk.
ALIYEKO HATARINI ZAIDI:
1. Watu wanaofuga wanyama mwitu ama wanaoishi katika maeneo yenye wanyama mwitu,
2. Watu wanaotegemea wanyama mwitu na ndege kama chakula chao;
3. Watumishi wa vyumba vya kuhifadhia maiti- hasa miili ya waliokufa kwa Ebola,
4. Watumishi wa hospitalini na wauguzi wanaowahudumia wagonjwa wa Ebola,
6. Wanafamilia wa wagonjwa wa Ebola,
7. Watu wanaohudhuria hospitali ambazo hazina mazingira safi na salama, nk.
NAMNA YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA EBOLA
1. Epuka kugusa damu/majimaji ya wanyama ama binadamu walio na ugonjwa wa Ebola au hata maiti za watu waliokufa kwa ugonjwa huo kwa kuzingatia haya:
a) Mazingira ya hospitali yawe safi na salama kila wakati,
b) Watelekeze wagonjwa wa Ebola,
c) Fukia miili ya waliokufa kwa Ebola kwa usalama,
d) Epuka mazishi ya kienyeji kama kuosha maiti za watu waliokufa kwa Ebola, nk.
2.Watumishi wa afya na waugizi wa wagonjwa wa Ebola wanatakiwa kuzingatia haya:
a) Kuvaa kwa usahihi vifaa vya kujikinga na nyuso, mikono na macho,
b) Kuvaa majoho maalum wakati wote wakiwa wanawahudumia waathirika,
c) Kutumia sindano mara moja na kuziteketeza ama kuzifukia,
e) Epuka kuosha maiti za watu waliokufa kwa Ebola, nk.
Namna ambavyo wauguzi na watoa huduma kwa wajonjwa wa Ebola wanavyopaswa kuvaa |
***Share na wenzako ujumbe huu
Sign up here with your email