JINSI YA KUPATA MAPENZI UNAYOTAKA KATIKA NDOA.

JINSI YA KUPATA MAPENZI UNAYOTAKA KATIKA NDOA.

Mkiwa kwenye uhusiano,ni suala la msingi sana kujua namna ya kufanya ili kupeana raha,kwa sababu hakuna mtu anayeingia kwenye ndoa kusaka mtu wa kumtukana matusi au kumpiga.
Je,mpenzi wako unamfanyaje? Kila mwenye mpenzi anapaswa kujiuliza mwenyewe.Wako wanaune ni madikteta,anamburuza mke kadri anavyotaka,wala hajali hisia zake,kitu ambacho ni kibaya.
Kuna wanaume wanafikiri wanawake ni kama gunia unamfanyia vituko na matusi unavyotaka,unamnyanyasa au kumsema kwa watu kadri unavyotaka,kitu ambacho si sahihi.Kuna wanaume wengine licha ya kutambuliwa kama vichwa vya nyumba,akikwaruzana na mwenziwake,anachokijua ni kununa,kususa au hata kulala sebuleni,hii ni akili ya kitoto.Mume kama kichwa cha nyumba,kinapaswa kuwa mfano wa kuigwa,kila mwanaume anapaswa kujiangalia matendo yake.
Lakini pia kila mwanamke anapaswa kuangalia matendo yake anayofanya kwa ndoa yake na kwa mumewe. Je,ni matendo ya haki? Kila mwenye akili timamu anapaswa kufanya vitu ambavyo yeye akifanyiwa,atajihisi kupata raha.Jiulize wewe mwenyewe,je,unayofanya ni mambo ya aina gani?. Wakati mwingine tunakuwa na ndoa mbaya kwa sababu ya matendo ambayo tunatenda.
Ni lazima uwe makini kwa vitu ambavyo unafanya.Lakini ni muhimu katika uhusiano kuwa na kawaida ya kuwa na muda wa kutafakari kwa umakini mkubwa hali ya ndoa yako na kuona ni yapi yanakwenda hovyo au yanakwenda safi.Katika maisha msingi wa kuwa na maendeleo mema,ni kuwaza na kufanya mema,ndio kusema hata kama labda ndoa yako ina matatizo,unapaswa kuwaza namna ya kufanya mema kwa maana ya kuondoa kasoro zilizoko na kadhalika.

Ni ujinga 
kutarajia mazuri kwenye ndoa yako wakati hufanyi mazuri,utakuta labda mwanume anarudi nyumbani usiku wa manane akiwa amelewa au kutokea kwenye uzinzi,halafu bado anatarajia mema kutoka kwenye ndoa yake,inawezekanaje? Ni suala lisilowezekana.Utakuta mwanamke au mwanaume ni jeuri,utakuta mwanaume halali nyumbani,labda kaporwa na shugamami,lakini bado anatarajia maisha yake yawe na faraja,kitu kisichowezekana.Kukubali kuacha ndoa yako,ni dalili kuwa haupo sawa.
Ni ujinga kukimbilia mwanamke au mwanaume mwingine na kuacha ndoa yako,kwa sababu hayupo ambaye hana kasoro.Kama unafikiri yuko mwanaume au mwanamke ambaye hana kasoro,jua kuwa fikra zako haziko sawa.Kwa ufupi ni kwamba katika kila ndoa,kuna wakati kunatokea hitilafu,cha msingi ni kukaa chini na kuondoa kile ambacho kinaleta shida.Cha msingi ni kwa watu kuacha kudharau,kuachs majivuno,kuacha kuona kwamba aaah nikimuomba msamaha ataona najikomba,hakuna ubaya kuitwa unajikomba ikiwa unachokitaka ni kizuri kwa ndoa yako.
Ndoa nyingi zinaharibiwa kwa sababu ya wanaume wanashindwa kuzingatia majukumu yao,mwanzo wa uhusiano wao kutofahamu huyu ni mwongo au mkweli.Kwa mfano tatizo la nguvu za kiume ambalo linaonekana kusumbua wengi,linaweza kutibika kwa kutumia mchanganyiko wa vyakula kama ambavyo nmewahi kueleza mara kadhaa,huna sababu ya kulia.
Ninachotaka kusisitiza hapa ni kwamba mojawapo ya namna ya kupata unachokitaka katika mapenzi,ni kumfanyia mwenzi wako mambo mazuri.Unapaswa kujifunza zaidi ili kuwa na ndoa nzuri zaidi,unapaswa kumjua mwenzi wako anataka nini na kisha kufanya yale ambayo unafikiri kwamba ukimfanyia atakuwa mwenye furaha.
Kila ndoa ina matatizo,na yanaweza kufumuka wakati wowote.La muhimu ni kwamba unapokuwa umeamua kujiingiza katika maisha ya ndoa unapaswa kujifunza jinsi ya kukabiliana na matatizo hayo ili yaweze kuisha salama na ndoa kuendelea kuwa salama.
Previous
Next Post »

Blogger templates