MATUKIO 9 YALIYOFURAHISHA

MAKALA: gladness mallya
Ijumaa iliyopita ni siku ambayo haitasahaulika kwenye kumbukumbu za wengi kutokana na kufanyika kwa tamasha kubwa la Usiku wa Matumaini ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yafuatayo ni mambo tisa yaliyotingisha kwenye tamasha hilo.
Ali kiba wa Bongo Fleva akimtoka 'Cloud' wa Bongo Muvi.
MECHI YA BONGO MUVI  VS BONGO FLEVA
Timu hizo zilipoingia uwanjani kupasha misuli, watu walisimama na kuanza kushangilia kwa nguvu huku wakilitaja jina la Ali Kiba na zaidi walifurahi walipomuona Jacob Stephen ‘JB’. Matokeo ya mechi hiyo, Bongo Fleva waliwalaza Bongo Muvi kwa  bao 1-0.
Wasanii wa Bongo Muvi wakicheza kiduku.
VIDUKU VYA BONGO MUVI
Japokuwa walifungwa, wanawake wa Bongo Muvi walionekana wakicheza kiduku huku mashabiki wakiwashangilia kwa nguvu na kuleta shangwe za aina yake.
'Sir Nature' akifanya makamuzi.
SHOO KALI YA ROMA, JUMA NATURE
Wakali hawa wa muziki wa Bongo Fleva waliwafurahisha sana mashabiki ambapo uwanja mzima ulisimama na kucheza huku wakiimba nyimbo za wasanii hao wakati wakipafomu.
'Cloud' akimbwaga 'JB' ulingoni.
NDONDI ZA JB, CLOUD
JB na Cloud 112 walionekana kama wanaigiza kwani walikuwa wanadondoka mara kwa mara wakati pambano baina yao likiendelea, baadaye JB aliibuka na ushindi.
Mashabiki wakifuatilia shoo uwanjani.
MASHABIKI KUSHANGILIA KWA STAILI MBALIMBALI
Ukweli ilikuwa ni siku ya matumaini na furaha kwani mashabiki kila mmoja alikuwa akishangilia kwa staili yake, wapo waliovua mashati na kubaki tumbo wazi huku wakicheza, wapo mashabiki wa kiume waliokuwa wanakata mauno kama wanawake na kuwa kivutio kikubwa uwanjani hapo.
Shilole 'akiangusha mauno'.
SHILOLE KUTAKA KUVUA NGUO
Hii ilikuwa ni hatari kwani mwanadada wa muziki wa mduara , Zuwena Mohamed ‘Shilole’ alifanya shoo ya nguvu lakini wakati anataka kufika mwisho akataka kuvua nguo kutokana na mzuka aliokuwa nao kwani alikuwa akiimba ‘nivue muone’ mashabiki nao wakawa wanaitikia ‘vua’, watu walipiga kelele za furaha kutokana na kufurahishwa na shoo ya mwanadada huyo.
Shabiki aliyejipenyeza uwanjani na kumganda mheshimiwa Mwigulu Nchemba kwa shangwe nyingi.
SHABIKI KUMGANDA MBUNGE
Ukiwa na mapenzi na kitu hutaona aibu! Baada ya wabunge kumaliza mechi shabiki mmoja alipenyeza uwanjani na kumganda mheshimiwa Mwigulu Nchemba huku akiwa amevua shati na alipokuwa akizunguka naye uwanjani alikuwa akifika sehemu anapiga magoti kwenye miguu ya mheshimiwa huyo na kunyoosha mikono juu na kuwa kivutio kwa watu waliokuwepo uwanjani hapo.
Yemi Alade akiulizia uwepo wa Johnnny kabla ya 'kupafomu'.
SHOO YA KIBA, YEMI FUNGA KAZI
Baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba kufanya shoo ya nguvu alifuatiwa na mwanadada huyu kutoka Nigeria, Yemi Alade ambapo mashabiki walifurahia kwani walikuwa wamemsubiri kwa muda mrefu.
Alikiba akipafomu huku Steve Nyerere akisindikiza shoo kwa kiduku.
ALI KIBA KUBEBWA
Kutokana na kufanya shoo nzuri, Ali Kiba alijikuta katika mikono ya msanii wa muziki na filamu, Simon Mwapagata ‘Rado’ ambaye alimbeba na kumzungusha uwanjani hapo huku akiimba, ukweli ilikuwa noma sana!
Previous
Next Post »

Blogger templates