SANDRA ATOKA NDUKI KISA AIBU

Stori: Shani Ramadhani
MSANII wa filamu Bongo, Salma Salmini ‘Sandra’ alijikuta akitoka nduki katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar kwa kukwepa aibu baada ya timu yao ya Bongo Movie Unity kufungwa na Bongo Fleva bao mbili bila.
Msanii wa filamu Bongo, Salma Salmini ‘Sandra’
Sandra alionekana akitimka mapema uwanjani baada ya mechi kuisha huku akisema anaona aibu kupokea kipigo hicho ambacho kimejirudia mara ya pili kwani mwaka jana kwenye mechi kama hiyo ya Tamasha la Usiku wa Matumaini, wapinzani wao hao waliwatandika bao 2-1.
Mwanamuziki H-Baba akiwatoka wachezaji wa Bongo Movies.
“Tumefungwa na Bongo Fleva ndiyo mashindano hatuna budi kukubali ila siwezi kuendelea kutazama burudani nyingine zinazoendelea, ni aibu tutazomewa sana,” alisema Sandra.
Previous
Next Post »

Blogger templates