Haruni Sanchawa na Makongoro Oging’
BINTI mmoja aliyefahamika kwa jina la Suzana Adamu (20), mkazi wa Mazizini- Ukonga jijini Dar amefariki dunia kwa kugongwa na gari akitoka kukamilisha taratibu za viza kwa ajili ya kwenda Dubai kufanya kazi.
BINTI mmoja aliyefahamika kwa jina la Suzana Adamu (20), mkazi wa Mazizini- Ukonga jijini Dar amefariki dunia kwa kugongwa na gari akitoka kukamilisha taratibu za viza kwa ajili ya kwenda Dubai kufanya kazi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, ilitokea Agosti Mosi, mwaka huu saa 2:30 usiku katika Mtaa wa Mahita ambapo mrembo huyo alikuwa akitoka mjini kwa ajili ‘shoping’ pia kuaga ndugu na jamaa ili kesho yake apande ndege kwenda Dubai ambako alipata kazi ya mkataba wa miaka miwili.
Ndugu na jamaa wakiomboleza msiba huo.
Ndugu na jamaa wakiomboleza msiba huo.
Ilidaiwa kuwa, akiwa anarudi nyumbani kwao, alipofika eneo hilo alizolewa na gari lililokuwa limekodiwa na watu waliokuwa wanatoka ufukweni kula Sikukuu ya Idd.
Mashuhuda walisema dereva wa gari hilo alikuwa mwendo kasi na hivyo kumvaa binti huyo aliyekuwa akitembea kwa miguu.Imeelezwa kuwa, kutokana na mwendo kasi, baada ya kumgonga Suzana gari hilo lilikwenda kugonga ukuta.Mwili wa marehemu ukishushwa kwenye gari nyumbani kwao.
Akizungumza na Amani kwenye msiba wa binti yake, baba mzazi wa mrembo huyo, Adamu Mohamed alisema siku ya maziko ya marehemu huyo ndiyo ilikuwa safari yake ya kwenda Dubai.
“Ndugu mwandishi, kaburini ndiyo Dubai ya mwanangu. Sasa si mkataba tena wa miaka miwili bali amepata mkataba wa kudumu huko alikokwenda,” alisema mzee huyo kwa masikitiko.
Alisema Suzana ni mtoto wake wa nne kuzaliwa, amemuacha katika wakati mgumu kwa sababu alikuwa tegemeo kubwa ndani ya familia. Marehemu Suzana alizikwa Agosti 2, mwaka huu katika Makaburi ya Kijiji cha Mfuru, Kata ya Maneremango, Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
Mmoja wa marafiki wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha, alisema kifo cha Suzana ni pigo kubwa kwao kwani alikuwa mkarimu aliyependa kuwasaidia wenzake.
Sign up here with your email