DUNIA INA MAMBO: DAWA YA KUKAMATA WEZI YAZUA BALAA...WAHUSIKA WAPAGAWA NA KUANZA KULA NYASI!

Watu saba kati ya 100 Kijiji cha Kenyamanyori, Kata ya Turwa, Wilaya ya Tarime walioshiriki kunywa dawa ya mganga wa kienyeji aliyeletwa kutoka Busia nchini Kenya wameingia kwenye wakati mgumu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kulipa Sh3 milioni kila mmojaWanakijiji hao walikusanyika juzi asubuhi baada ya kengele ya kijiji kugongwa na uongozi, huku wakieleza kwamba ilikuwa siku ya nne kwa kengele hiyo kugongwa lengo
likiwa ni kuzungumzia wizi unaoendeshwa na watu wasiojulikana.Inadaiwa wizi wa kuvunja maduka umekithiri kijijini hapo, baada ya wanakijiji hao kuwasili eneo la mikutano, walielezwa kusudio la kengele kuwa ilikuwa ni kutokana na kukithiri kwa matukio ya uhalifu.


Miongoni mwa waliovunjiwa duka ni Ayubu Wambura, anayedaiwa kuleta mganga kutoka Busia nchini Kenya kuwabaini wahusika, hivyo kila mmoja aliombwa kunywa dawa ya mganga huyo au kuacha maana ni hiyari.
Previous
Next Post »

Blogger templates