Stori: Mayasa Mariwata na Shani ramadhani
WIVU wa mapenzi bwana! Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la David Patrick Chagu (pichani) aliyekuwa akiishi Jimbo la George nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ amekumbwa na mauti kwa kuchomwa visu na mpenziwe aliyefahamika kwa jina moja la Monica.

Tukio hilo lilitokea Oktoba 2, mwaka huu na marehemu alizikwa Oktoba 14, mwaka huu katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar huku akiwa ameacha mtoto wa miezi nane.
Kwa mujibu wa chanzo, marehemu alichomwa visu na mpenzi wake huyo ambaye ni Mzungu kwa madai ya wivu kufuatia kutomwona kwa siku tatu na kumhisi ana mpenzi mwingine.
Akizungumza na Uwazi kwa majonzi makubwa, mama mzazi wa marehemu, Rose Ndunguru ambaye ni Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Kata ya Ubungo alisema alipatwa na simanzi kubwa kutokana na kitendo hicho alichokifanya mkwewe ambaye alikuwa akimpenda mno na kutoamini alichomtendea mwanaye.
“Naumia sana jamani sijui nielezeje! Chanzo cha yote Monica alinipigia simu akasema ana siku tatu hajaonana na David kwa kuwa walikuwa hawaishi wote.“Alisema nimpigie simu David, nimwambie mtoto anaumwa, ndipo mwanangu akaenda na kumkuta mtoto mzima isipokuwa alikuwa akisumbuliwa na mafua.”
“Siku iliyofuata, kwa kuwa David ni mfanyabiashara mbali ya kuwa ni mwanafunzi katika Chuo cha Wescaptown, akiwa anatoka kwenye biashara zake alikwenda nyumbani kwa Monica kumrudisha shemeji yake wa kiume akiwa na gari.
“Aliposhuka tu akiwa eneo la wazi la barabara ndipo Monica akamchoma visu vitatu, kifuani na cha mkononi bila huruma,”alisema mama huyo.Aliongeza kuwa, kutokana na tukio hilo ambalo lilitokea usiku wa Alhamisi mwanaye alikimbizwa kwenye Hospitali ya Mozaribay iliyopo palepale George, lakini baada ya nusu saa akafariki dunia.
“Monica alikamatwa asubuhi yake na kuwekwa ndani japo mpaka sasa yupo nje kwa dhamana.
“Inasikitisha sana kwani sasa amekuwa akinisumbua kwenye simu akitaka matumizi ya mtoto na kuniambia nimsamehe kwa alichofanya kwani hakukusudia.”Mama huyo alisema yeye ameshamsamehe Monica kwa yote yaliyotokea na kumwachia Mungu.

Sign up here with your email