11 wadaiwa kufariki kwenye ajali ya basi na daladala Mwanza

Watu 11 wanadaiwa kupoteza maisha na wengine 10 kujeruhiwa kwenye ajali basi la Super Shem lililogongana na daladala linalofanya safari zake Nyegezi na Shilima kwenye eneo la Hungumalwa mkoani Mwanza alfajiri ya leo.
whatsappimage2016-09-21at09-38-31
Basi la Super Shem lilikuwa likitokea mkoani Mbeya kuelekea Mwanza, liligongana na daladala hiyo ambayo iliingia kwenye barabara kubwa bila ya kujua kuwa nyuma yake basi hilo linakuja kwa mwendo kasi.
whatsappimage2016-09-21at09-38-35
Abiria wanaodaiwa kupoteza maisha na kujeruhiwa zaidi ni wale walikuwa kwenye daladala .
whatsappimage2016-09-21at09-38-33
Hii ni ajali kubwa ya pili inayohusisha basi la abiria kutokea ndani ya wiki hii ukiacha ile iliyotokea mkoani Njombe na kuua watu 12 siku mbili zilizopita.
Picha: Michuzi
Hizi ni picha zingine za ajali hiyo.
7b80a97b-5ba3-4055-8c63-27eb3615e468
738c44e2-d30e-4081-900e-ada508e43389
1062be22-87ac-4dff-ac7c-23f79b9507ca
18783096-2398-45ac-bf72-b3316b6884cc
d7022c30-82c1-4783-b427-e25755d78e43
f5bb4974-bdba-4add-8241-426b57d5f7d3
f6b4ecea-3dcf-47ac-9050-3549206ca13b
Previous
Next Post »

Blogger templates