Mwanamke mmoja ambaye alikuwa na ujauzito nchini Pakistan amepigwa mawe hadi kufa nje ya jengo la mahakama kwa kosa la kuolewa na mwanaume anayempenda badala ya mwanaume aliyechaguliwa na familia yake.
Hatma ya mwanamama huyo Farzana Parveen, 25 inawakumba wanawake wengi nchini Pakistan na katika nchi nyingine.
Aliuwawa kwa kuiabisha familia yake ambapo mauaji hayo yamefanywa ambapo hata ndugu wa familia yake wameshiriki katika tendo hilo lililokemewa na Umoja wa mataifa.
Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa mwezi April mwaka huu na Tume ya haki za binadamu nchini Pakistan inasema kwa wanawake 869 nchini humo wamekuwa wahanga wa matukio ya aina hiyo na wanaharakati wanasema idadi hiyo inaweza kuwa iko juu zaidi.
Sign up here with your email