Historia ya Mitaa mbali mbali ya Jiji la Dar Es Salaam Kwa nini iliitwa majina hayo? Azikiwe, Samora, Pamba, Garden, Mkwepu, Makunganya, Shauri Moyo, Jamhuri, Uhuru, Kongo...YOTE HAPA

Nnamdi Azikiwe alikuwa ni kiongozi wa kwanza wa Nigeria mara baaya uhuru wa nchi hiyo. Barabara yetu ile maarufu imepewa jina hilo kama kumbukumbu yake. Alifariki mwaka 1996.


Samora Machel naye, kama Azikiwe, alikuwa ni kiongozi wa Msumbiji aliyepinga utawala wa amakaburu wa Afrika Kusini. Alifariki kwenye ajali ya ndege mwaka 1986. Mjane wake ndio mke wa Mandela wa sasa. 

Hassan Omari Makunganya alikuwa kiongozi wa Wangindo (sina uhakika sana na kabila). Aliongoza watu wake kupigana na Wajerumani dhihi ya utawala wa Wajerumani. Alishirikiana na akina Kinjekitile Ngwale katika vita iliyojulikana kama Majimaji (1905 - 1907)

mtaa wa Lindi...
Mtaa huu ndio mrefu kuliko mitaa yote hapa Dar.

Mtaa wa Agrey...
Huu ni mtaa wa pili kwa urefu Dar.

Mtaa wa Congo...
upo Kariakoo.
Huu ni mtaa ambao una pilika na Tashtiti kuliko mitaa yote Tanzania.
Halahala, Mtaa huu ukijishaua kuzubaa tu unaibiwa.

Mtaa wa Sikukuu...
Mtaa huu ni mtaa unaouza madiko diko usiku kucha.
Nenda muda wowote mtaa huu utapata Chakula.
huu pia uko Kariakoo.

Mtaa wa Chui...
Pia nao upo Kariakoo.
Ni mtaa unaoaminika kuwa na walaji Mirungi kuliko mtaa wowote Dar es Salam.

Mtaa wa Pemba...
Upo Kariakoo.
Umelaaniwa, hauna Lami.
kwa taarifa yako mtaa huu unapita katikati ya soko kuu la Kariakoo. 

Mtaa wa Swahili.
Huu mtaa upo Kariakoo.
Mtaa huu unaanzia Kariakoo Shimoni unaishia Gerezani.

Mtaa wa Twiga.
Upo Kariakoo.
Ndipo lilipo jengo la club yenye mafanikio zaidi hapa nchini.
Hapa naizungumzia club ya YANGA.

Itaendelea...
Previous
Next Post »

Blogger templates