Mwimbaji Justin Bieber ambaye jana alitawala vichwa vya habari baada ya kurushiwa makonde na muigizaji Orlando Bloom kwa ajili ya mrembo Miranda Kerr, ameonesha jinsi alivyo na kisu kirefu zaidi kwa watoto wazuri.
Bieber ameonekana akila bata kwenye yacht katika eneo la Ibiza na mrembo wa Australia anaefahamika kwa jina la Shanina Shaik.
Shanina Shaik ambaye ni mwanamitindo maarufu alipost baadhi ya picha kwenye Instagram akiwa na Justin Bieber.
Mrembo huyo aliwahi kuwa mpenzi wa mwanamitindo maarufu wa Marekani ambaye pia ni muigizaji, Tyson Beckford kwa miaka mingi na uhusiano wao ulivunjika mwaka jana.
Sign up here with your email