Bodaboda wamkera LOWASA mara baada ya kumwita Rais....

 WAZIRI Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa juzi Jumapili alitibuliwa na waendesha pikipiki (Bodaboda) wa wilaya zote za  jijini Dar Salaam katika Viwanja wa Leaders baada ya kusukuma gari lake huku wakiimba ‘rais, rais, rais. 

Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli alionekana kutibuka alipopewa nafasi ya kuzungumza  katika mkutano huo uliokuwa maalum kwa ajili ya kuzindua saccos ya waendesha bodaboda ambapo alisema wanaomwita rais wanataka kumkosanisha na watu.
Hata hivyo, hakusema anataka kukosanishwa na nani.
Lengo la kuanzishwa kwa Saccos hiyo ni kuwasaidia waendesha bodaboda kujiongezea kipato na kujinunulia pikipiki zao na kuachana na kuendesha pikipiki za matajiri.

Edward Lowassa akiongea na waendesha bodaboda (hawapo pichani)

Lengo langu mimi ni kutaka kuwaona mmejiajiri kwa kuendesha pikipiki zenu wenyewe si za matajiri hivyo ni vizuri kuanzisha Saccos ambazo zitawasaidia kujikwamua na kuendesha pikipiki za matajiri,” alisema kiongozi huyo ambao walizidi kushangilia kwa nguvu ‘rais… rais..rais.
Jamani hizo kelele za rais, rais, mtanigombanisha yaani mnanichonganisha na watu,” alisema Lowassa.
Baada ya uzinduzi wa Saccos yao, Lowassa aliondoka viwanjani hapo huku gari lake lilisukumwa na waendesha bodaboda hao ambao waliendelea kuimba ‘rais… rais’ na kuwapa kazi kubwa polisi ya kuwatawanya


Read more: http://mambomseto88.blogspot.com/2013/12/bodaboda-wamkera-lowasa-mara-baada-ya.html#ixzz2nkSqMscA
Previous
Next Post »

Blogger templates