ALICHOKISEMA STARA TOMAS KUHUSU KUFANYA NYIMBO ZA INJILI NA BONGO FLAVA KWA PAMOJA


DSC_0049Ni zaidi ya mwaka mmoja tangu Stara Thomas atangaze kuachana na muziki wa bongo fleva na kuokoka na kuamua kufanya muziki wa dini,tayari kuna baadhi ya nyimbo za Bongo fleva  ambazo ndani yake  inasikika sauti yake na kuna taarifa kuwa ni member wa kundi la VOA ambalo ndani yake yupo Linex.
Stara Thomas amelielezea kwa usahihi juu ya jambo hili>>’Kiukweli muziki wa bongo fleva baada ya mimi kuokoka na kuingia moja kwa moja kwenye muziki wa Gospel,Bongo fleva nitakuja kuifanya kwenye kuelimisha jamii,kuelimisha wanafunzi na kuelimisha hata wenyewe wanaofanya bongo fleva’
‘Baada ya kukaa vizuri ndani ya biblia nimekuja kuona naweza kufanya bongo fleva lakini zipo njia njema ambazo naweza kushiriki kwenye bongo fleva vizuri lakini lile suala la matamasha kidogo nimeliona linasumbua kwa sababu unakua kwenye mazingira ambayo wewe uliyozoea kuwepo katika madhabahu ya bwana na kusimama kwenye maeneo fulan ambayo watu wanakunywa pombe au wako kwenye mazingira ambayo c mazuri’
‘Kwa sasa tunajaribu kuangalia tunafanyaje sisi watu wa Gospel kuingia kwenye maeneo hayo na kuweza kuwafundisha haijalishi kama kuna bongo fleva pamoja na kwamba kuna maisha yanayoendelea hapo lakini ni vyema tukaishi tukiwa tunatafakari matendo makuu ya Mungu’.

Previous
Next Post »

Blogger templates