ODAMA APIGA MZIGO NA UJAUZITO WAKE

MTOTO mzuri Bongo Movies, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amesema japokuwa ni mjamzito lakini bado ana kasi zaidi katika kufanya kazi zake za filamu. 
Jennifer Kyaka ‘Odama’.
 Akipiga stori na paparazi wetu, Odama alisema watu wengi wanaamini unapokuwa mjamzito unaacha shughuli zako lakini kwake mambo ni tofauti, kazi kama kawaida.
 “Mimi mzigo hapa naendelea kama kawaida wala mimba siyo kigezo cha kusubirisha  mambo yangu, kwanza naona ndiyo imenipa nguvu ya kufanya kazi zangu, nimekamilisha tayari kazi mpya, naiachia March 28 inaitwa Jicho Langu,” alisema Odama.
Previous
Next Post »

Blogger templates