Hii ni taarifa kutoka Kenya ambapo inasemekana Wazazi katika kaunti ya Kirinyaga mkoa wa Kati nchini Kenya wameandamana kwa hasira baada ya mwalimu mmoja kumchapa mtoto mmoja wa shule ya msingi hadi kupoteza maisha.
Mtoto huyo inasemekana alichapwa kichwani na mwalimu na kuzirai na alipokua akipelekwa hospitali alifariki dunia,ambapo wazazi hao wameandamana kwa amani wakitaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.
Polisi nchini Kenya wamemtia mbaroni tayari mwalimu huyo na kwa sasa anashirikiwa na Polisi huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufanywa,Mtoto huyo alikuwa katika darasa la saba katika shule ya kibinafsi iitwayo Roka Preparatory.
Wengi wa wazazi wenye watoto wao katika shule hiyo wameahidi kuwahamishia shule nyingine ambapo Nchi ya Kenya iliharamisha kitendo cha kuwachapa wanafunzi wa shule karibu miaka kumi iliyopita na hii ilikuwa baada ya visa vya walimu kuwaadhibu vikali wanafunzi na kuwajeruhi kukithiri.
Source:Bbc Swahili
Sign up here with your email