HUYU NDIYE M’BONGO ALIYEMBWAGA PREZZO...SASA INADAIWA ANATOKA NA DAVIDO.

Muite Chagga Barbie,hivyo ndivyo kila mtu amjuavyo kwa jina lake hilo maarufu,mrembo huyu kutoka hapa bongo,anayeishi nchini Marekani,ndiye aliyekuwa anatoka na mkali wa muziki kutoka nchini Kenya,Prezzo na kama ilivyo kawaida ya watu maarufu wengi, mahusiano yao hayakuweza kudumu,mwisho wa siku kubwagana tena kwa kurushiana maneno kupitia mitandao ya kijamii, ikiwemo twitter,ila baada ya muda ilijulikana kuwa waliweza kusuluhisha msala wao,ila hiyo haikuwa ishu.
collagesfd
Sasa baada ya mkasa huo wakubwagana na Prezzo,Mrembo huyu alionekana ku-spend muda mwingi na Davido, msanii maarufu kutoka nchini Nigeria ,wengi wakimjua kama mkali wa skelewu,walionekana pamoja wakati wa concert ya Davido, iliyofanyika huko mji wa  Minneapolis nchini marekani,na mashabiki wengi kubaki kujiuliza maswali mengi kama ndiyo tumepata shemeji m’Nigeria hivi sasa hivi au la?.
Davido ametokea kuwa ni moja ya wasanii wakubwa Africa,ameweza kushinda tuzo mbali mbali zikiwemo,Kora Award,  Channel O Music Video Award,  Nigeria Music Video Award, tuzo tatu za The Headies awards, tuzo nne Nigeria Entertainment Awards, na tuzo mbili za Dynamix All Youth Award katika muda mchache tu toka aanze ku-make headlines kupitia nyimbo yake ya skelewu,iliyompa umaarufu mkubwa duniani.

Previous
Next Post »

Blogger templates