DIAMOND PLATNUMZ KUFANYA VIDEO NYINGINE MPYA NCHINI UINGEREZA


Diamond Platnumz anazidi kudhihirisha kuwa yeye ni mfano wa kuigwa kutokana na jitihada kubwa anazozifanya za kujiimarisha na kujitangaza katika soko la Afrika. Baada ya kufanya collabo na baadhi ya wasanii wa Nigeria aliko hivi sasa, ameweka wazi mpango wake wa kufanya video nyingine nchini Uingereza. 

Platnumz ambaye amefanikiwa kufanya collabo na Kukere master Iyanya, amesema mara atakaporejea Tanzania ana mpango wa kwenda nchini Uingereza kufanya video ya wimbo wa pili, sababu anampango wa kutoa nyimbo mbili mwaka huu moja ikiwa ni kwaajili ya soko la nyumbani na ya pili kwaajili ya soko la Afrika.
 
“Nikitoka Nigeria Inshallah nikirudi nitaenda Uingereza kushoot ngoma nyingine” Diamond Aliiambia Amplifaya ya Clouds Fm. “Kwasababu nimeplan mwaka huu kutoa nyimbo mbili ambayo ya kwanza itakuwa East African version nyingine itakuwa Kiafrika kwasababu ukitaka utoe hit nzuri ya Afrika au ya West na sehemu nyingine ni ngumu sana kupeleka ile kama tunavyoimba sana nyumbani lazima kidogo ubadilike na ukibadilika unajua watanzania wanakuwa hawakukubali hivyo so inabidi nifanye hivyo.”
 
Pia Diamond amesema video anayotarajia kuifanya nchini Uingereza ni ya wimbo aliomshirikisha Iyanya.
 
Wakati platnumz anaondoka Tanzania kuelekea Nigeria alisema moja ya vitu atakavyovifanya huko ni pamoja na kufanya video nyingine, na kuongeza kuwa itakuwa ni ya wimbo alioimba mwenyewe japo hakutaja jina wala siku itakayotoka lakini alithibitisha wimbo mpya utatoka hivi karibuni.
 

Diamond atakuwa msanii wa pili wa Bongo kufanya video nchini Uingereza kwa mwaka huu kama mipango hiyo itaenda kama ilivyopangwa, baada ya Ommy Dimpoz ambaye ameshoot nchini humo hivi karibuni.
Previous
Next Post »

Blogger templates