DAZ BABA AKANUSHA KUTUMIA BANGI NA MADAWA MENGINE YA KULEVYA ....ADAI BADO YUPO PHYSICALLY AND MENTALLY FIT

 
Msanii wa zamani wa kundi la Daz Nundaz, Daz Baba amesema kuwa hatumii madawa ya kulevya kama watu wengi wanavyodhani. 

Muimbaji huyo ambaye wiki hii ameachia wimbo mpya uitwao ‘Jela’ amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa yupo fit kuendeleza gurudumu lake la muziki.
 
“Kikumbwa mashabiki wangu wajue zile habari walizokuwa wanazisikia kwenye magazeti ni uzushi tu,” alisema.

 “Kwahiyo waelewe mimi bado nipo fit mentally, yaani kila kitu,ndio maana hata sasa hivi nimeweza kuzungumza.Watu walikuwa wanatafuta mchongo wa wao kusikika,mimi nikiwa fit nasikia kuna mtu ananizungumzia,kwahiyo nilikuwa naona kwa chini kuna beef fulani,sasa mtu anakuwa na beef anashindwa kuongea? Kawaida sisi marasta tunapenda kuambiana live, wewe kama una kinyongo unachana.

"Watu waelewe Daz Baba hatumii madawa na ni mwiko kwangu mimi. Kwanza ni rasta na unajua sisi tuna imani rasta ni upendo, sasa kama una upendo lazima ujipende mwenyewe, wewe huwezi kumpenda mtu kama mwenyewe hujipendi utakuwa mnafiki.

 "Siwezi kutumia unga wakati mimi najua una madhara watu wanapinga halafu nije kutumia drugs wakati nina malengo, afanya shule nini,nina familia, kwahiyo nilikuwa kimya kutokana na project ya Tanzaniano.”
 

Daz Baba ambaye ana watoto wawili mapacha,amewataka mashabiki wa muziki wake kuupokea kwa mikono miwili wimbo wake mpya ‘Jela’.
Previous
Next Post »

Blogger templates