SCENES ZA UCHI KWENYE FILAMU YA TITANIC BADO ZINAMSUMBUA KATE WINSLET AMBAYE ALIKUBALI KUSAULA NGUO ZAKE KWENYE FILAMU HIYO ILI LEONARDO DICAPRIO’ ALICHORE UMBO LAKE


Kate Winslet bado anasumbuliwa na scene yake ya uchi  kwenye filamu ya ‘Titanic.’ 

Mshindi huyo wa tuzo ya Oscar aliyeigiza kama Rose DeWitt Bukater, alisaula nguo zake kwenye filamu hiyo ya mwaka 1997 ili Leonardo DiCaprio’ aliyeigiza kama Jack Dawson alichore umbo lake tupu, anakubali kuwa hukosa amani kuangalia sehemu za filamu hiyo na hukataa kusaini picha zilizochorwa kuigiliza picha hiyo halisi.
Picha ya Rose iliyochorwa na Jack
Muigizaji huyo mwenye miaka 38 ameiambia Yahoo! Movies: “Huwa sisaini hiyo picha. Sijiskii amani. Kwanini nifanye hivyo? Watu huniambia nisaini picha hiyo sana.”

 

Muigizaji huyo kwa sasa ana mtoto wa kiume aitwaye Bear aliyezaa na mume wake Ned Rocknroll na wengine wawili aliowapata kwenye mahusiano yake ya mwanzo.
Previous
Next Post »

Blogger templates