Halima Kimwana alielezea sakata hilo wikiendi iliyopita baada ya kuulizwa undani wa skendo inayomkabili ya kumkuwadia au kumtongozea Diamond kwa mastaa na kuwabadilisha kama nguo.
Kwa mujibu wa Halima Kimwana, huwa Diamond hajisumbui kumtongoza mwanamke zaidi ya hao mastaa kujitongozesha wenyewe kwake.
Halima Kimwana alidai kwamba yeye kama dada wa mwanamuziki huyo (hakutaka kufafanua dada kivipi), amefikia hatua ya kusumbuliwa na wasichana wa kila aina hasa mastaa wakimuomba awatongozee kwa Diamond tena kwa ahadi kemkemu.
“Kwani unafikiri Diamond anajihangaisha kuwatongoza hao mastaa? Wao ndiyo kila kukicha wanamsumbua na kutuhangaisha sisi wakitaka tuwatongozee kwa kaka yetu.
Tena wengine wanatoa ahadi nyingi tu kama tukiwafanikishia,” alisema Halima Kimwana na kuongeza kuwa katika listi hiyo ya mastaa wanaojitongozesha kwa Diamond, wapo mastaa wakubwa ambao anawahifadhi ili asiwavunjie heshima.
Kama hiyo haitoshi, Halima Kimwana alianika kuwa, hajishughulishi na suala la uhusiano wa Diamond na atamheshimu kila msichana atakayetambulishwa KAMA WIFI HUKU AKITOLEA MFANO JINSI ANAVYOUHESHIMU UHUSIANO WA DIAMOND NA WEMA SEPETU KWA SASA.
Sign up here with your email