Awali, gazeti hili lilipokea ujumbe mfupi (SMS) kutoka kwa chanzo chake kuwa watu wa Ustawi wa Jamii wakishirikiana na polisi walitinga nyumbani kwa mama huyo na kumfikisha kituo cha polisi baada ya kufanya uchunguzi wa kina na kubaini ukatili aliokuwa akimtendea mtoto huyo.
Ilielezwa kwamba baada ya kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe, Dar, mlezi huyo alifunguliwa jalada la kesi namba CHA/RB/2245/2014- UKATILI DHIDI YA MTOTO ambapo anasubiri kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
Katika maelezo yake, mtoto huyo alidai kuwa amekuwa akipata vipigo vya nguvu kutoka kwa mlezi wake huyo ambaye alianza kumlea tangu akiwa na umri wa mwaka mmoja.
Huku akionesha majeraha sehemu mbalimbali za mwili, Sada alidai kuwa makovu aliyonayo yalitokana na fimbo anazotandikwa na mama huyo.
Kwa upande wake baba wa mtoto Athumani Francis (35) alisema yeye alikuwa hafahamu chochote kuhusiana na malezi hayo yasiyo sahihi kwa mtoto wake aliyekuwa akichoteshwa maji hadi ndoo kumi na tano kwa wakati mmoja, jambo lililowakwaza majirani.
Kwa upande wake Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, SACP Englibert Kiondo alisema suala la ukatili kwa watoto linazidi kushamiri kwa sasa hivyo wananchi wajitahidi kuonesha ushirikiano kwa kutoa taarifa katika vyombo
Sign up here with your email