Akizungumza na paparazi wetu, Dude alisema amewahi kubebeshwa unga na rafiki yake wa karibu ambaye hakumtaja jina na walikuwa wakitokea Nairobi nchini Kenya kuja Tanzania.Alisema wakati wanaanza safari alipewa koti la baridi na rafiki yake huyo, akalivaa kumbe ndani yake lilikuwa limeshonewa pakti za unga.
Walisafiri kwa gari na kila walipokutana na polisi wanaokagua hawakumkagua Dude kwani waliishia kupiga naye picha na kumsifia kwa kazi yake mpaka alipofika jijini Dar es Salaam.
“Kila tulipokuwa tunakutana na polisi rafiki yangu alikuwa akiwawahi na kuwaambia kwamba yupo na mimi ambapo walifurahia kuniona na kupiga picha na mimi bila kunikagua chochote,” alisema
Dude.
Baada ya kupita vizingiti vyote, waliingia jijini Dar es Salaam maeneo ya Kinondoni Manyanya alipokuwa akiishi rafiki yake huyo ambapo alimwambia avue koti, akaanza kufungua mzigo aliokuwa ameushonea kwa ndani.
Dude alijikuta akishikwa na tumbo la kuhara kutokana na mshtuko alioupata baada ya kuona rafiki yake huyo akitoa madawa ya kulevya.
“Jamaa alinipa shilingi elfu hamsini za Kenya na ni baada ya kufika Dar ndipo niligundua kwamba nilikuwa nimebebeshwa unga lakini yule jamaa alishakamatwa na anatumikia kifungo nchini Pakistani,” alisema Dude.
Hata hivyo Dude aliwashauri mastaa wenzake kuwa makini na marafiki zao kwani siyo wote wanaokamatwa wamebeba unga kwa kujua bali wengine
Sign up here with your email