Nahodha wa kikosi cha Real Madrid kitakachokuja hapa nchini, Ruben de la Red akithibitisha ujio huo.
Mkurugenzi wa TSN (T) LTD, Farouq Bahoza (kushoto) akibadilishana mkataba na Ruben baada ya kutiliana saini.
NYOTA wa zamani wa klabu ya Real Madrid ya Hispania, Luis Figo, Ruud Van Nistelrooy, Michael Owen na Fenando Hiero ni miongoni mwa mastaa watakaotua nchini kwa ajili ya ratiba mbalimbali, ikiwemo kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya kikosi cha Tanzania ‘XI stars’, mchezo utakaopigwa Agosti 23,mwaka huu.
Mbali na mchezo huo, pia nyota hao watakuwa na ziara ya kutembelea vivutio vya Tanzania, ikiwemo mbuga za wanyama kama Ngorongoro na kupanda mlima Kilimanjaro.
Ujio huo, ambao umedhaminiwa na Kampuni ya TSN, ambao wameingia mkataba leo na Real Madrid ya Hispania kwa ajili ya kuileta timu hiyo,, mwakilishi wa TSN Dennis Sebo, alisema kuwa msafara huo utakuwa na jumla ya nyota 25, huku wakitarajiwa kuwa na ziara ya siku tatu kabla ya kurudi kwao.
Sebo, alisema kikosi hicho kitawasili nchini Agosti 21 Alhamisi ambapo Ijumaa watakuwa na ziara ya kutembelea vivutio vya utalii, kama Ngorongoro na kupanda mlima Kilimanjaro kabla ya Jumamosi kukipiga na Stars na wataondoka nchini kesho yake (Jumapili).
Mbali na kina Figo, Sebo aliwataja nyota ambao wamekwisha thibisha kuwepo katika msafara huo kuwa ni pamoja na Fernando Morienties, Christian Karambeu, Steven McManaman, `Roberto Solgado huku Zidane Zidane itategemea na majukumu. Ni kocha msaidizi kikosi cha Madrid.
Sebo aliongeza kuwa Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, Iker Casillas na Sergio Ramos, watatu kati yao lazima wataambatana katika msafara huo.
“Tunatarajia kuwafuata Lisbon-Ureno kukutana nao kwa ajili ya kufanya tangazo la ziara hii, lakini pia wawili ama watatu kati yao wataungana na wataungana katika msafara huo.
“Figo ni kama yumo kwenye ndege anakuja, lakini kuhusu Zidane, ni kwamba itategemeana na majukumu yake. Kama hatokuwa ‘busy’ basi kuna uwezekano akaja, ila waliothibitisha ni hao waliotajwa (hapo juu),” alisema Sebo.
Kwa upande wa Real Madrid waliowakirishwa na kaptaini wa kikosi cha wakongwe hao Ruben de la Red aliishukuru TSN kwa kuwapa nfasi ya kufika Tanzania, ikiwa ni rekodi ya kipekee kwa kuwa nchi ya kwanza kuileta Real barani Afrika.
“Ni jambo la kipekee kwa TSN kuifanya timu yetu kukanyaga Afrika kwa mara ya kwanza, bahati imeangukia kwa Tanzania, hakika ni jambo la kuvunia.
“Tanzania ni moja ya nchi yenye mashabiki wa soka kwa wingi na amini kupitia mchezo huu dhidi ya vijana wa Kitanzania itakuwa sehemu ya kukuza na kuchota ujuzi fulani kutoka kwa timu kubwa kama yetu,” alisema Red ambaye pia ni kocha mkuu wa timu ya vijana ya Real Madrid.
Sign up here with your email