Saa
kadhaa kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, jamaa
aliyetajwa kwa jina moja la Lugali ameibua sekeseke kwenye nyumba ya
kulala wageni (gesti), kisa kikidaiwa ni mchepuko akihusishwa na mke wa
mpangaji wake, Ijumaa Wikienda lina kisa na mkasa.
Ilisemekana kuwa mume huyo alimweleza mkewe ili aamini kweli baba mwenye nyumba alipania kumtaka basi amkubali ili amkute naye gesti amkomeshe kwa tabia hiyo ya baadhi ya wenye nyumba ambao huwataka wake wa wapangaji wake.
Jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali akihusishwa kuchepuka na mke wa mpangaji wake, akiwa amenaswa kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar.
Wakati
ikirandaranda mitaani kutega mingo, Timu ya Oparesheni Fichua Maovu
(OFM) ya Global Publishers ilipokea mchongo kuwa kuna timbwili kwenye
gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar ambapo walifika eneo la tukio na
kushuhudia kasheshe hilo la aina yake.
OFM
ilimshuhudia mzee huyo akichomolewa kutoka chumbani huku damu
zikimvuja baada ya kula kichapo kutoka kwa jamaa na ndugu wa mwanaume
aliyedai kuwa jamaa huyo alikuwa anamsumbua mkewe.
Kwa
mujibu wa mashuhuda, kabla ya jamaa hao kuingia chumbani humo kwanza
walivunja mlango wa chumba hicho baada ya kupata idhini kutoka kwa
msimamizi wa gesti hiyo kufuatia baba mwenye nyumba huyo kukahidi
kuwafungulia mlango ili wamchukue mke wa ndugu yao aliyedaiwa kuwa ndani
na mzee huyo.
Walidai
kwamba mzee huyo ambaye ni baba mwenye nyumba, alikuwa akimtolea
udenda mke huyo wa mpagaji wake ambaye ni jirani yake huku akimsumbua
mara kwa mara kwa simu na ujumbe mfupi wa SMS.
Ilidaiwa
kwamba kufuatia usumbufu huo, mke huyo alimweleza mumewe lakini mumewe
hakuamini kama kweli baba mwenye nyumba alikuwa akimtaka mke wake
kimapenzi.Ilisemekana kuwa mume huyo alimweleza mkewe ili aamini kweli baba mwenye nyumba alipania kumtaka basi amkubali ili amkute naye gesti amkomeshe kwa tabia hiyo ya baadhi ya wenye nyumba ambao huwataka wake wa wapangaji wake.
Baada ya kukutwa gesti humo, mzee huyo aliomba msamaha kwa mpangaji wake huyo na kuahidi kulipa fidia ambapo aliwaandikia cheki feki kisha akakimbilia Kituo cha Polisi cha Buguruni na kufungua shauri kuwa alitekwa, akapigwa kisha akapelekwa gesti.
Shauri hilo ambalo liliandikishwa kwa jalada namba BUG/RB 6182/2014- utekaji. Mzee huyo alidai kutekwa na mpangaji wake huyo na kumpeleka nje ya mji kisha kumpiga ili kuua soo.
Hadi gazeti hili linaanua jamvi kituoni hapo, polisi walikuwa wakichunguza ili ukweli ujulikane.
Sign up here with your email