Mtoto mwenye umri wa miaka nane anadaiwa kulawitiwa na jamaa aliyetajwa kuwa ni mwendesha bodaboda.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni mjini hapa ambapo katika maelezo ya mtoto huyo wa kiume alidai kwamba, akiwa anatoka shule na mwenzake, njiani walisimama wakawa wanaokota matunda aliyoyataja kwa jina la ntalali.
Alisema ghafla mtuhumiwa alitokea na kumtaka mtoto huyo ampeleke nyumbani kwao kwa kuwa walikuwa wakifahamiana kabla ya hapo.
Mtoto alisema alikubali kuondoka na jamaa huyo hadi eneo la maficho karibu na mlima ndipo alianza kufanyiwa kitendo hicho.Baada ya kurejea nyumbani mtoto huyo alimweleza mama yake mzazi na kuanza harakati za kufika kituo kikubwa cha Polisi mjini hapa.
Hatua za kumkamata mtuhumiwa zilifanyika ingawa aliachiwa kwa dhamana jambo ambalo mama mzazi wa mtoto huyo amelilalamikia huku akidai kuwa huenda kuna hujuma dhidi ya kitendo kibaya alichofanyiwa mtoto wake.
Sign up here with your email