utofautisha kupendwa kweli na kutamaniwa.
Wapo walioingia mkenge kwa neno
hilo hasa walio wageni katika uwanja huu wa mahaba.
Ukiambiwa unapendwa basi unachanganyikiwa na kusahau maneno matupu hayajengi nyumba.
Nina maana gani? Watu wengi wamekuwa wakitumia neno hili kama mtego wa kumpata mtu, kwa kujifanya anakupenda sana na nahau nyingi za mapenzi ambazo zinaweza kukufanya masikio yako
yazibe na kuona nani kama wewe.
Siku zote mtafutaji ana lugha tamu ya mapenzi na kabla ya kutamka lolote lazima atangulize nakupenda sana na kuongezea ajuavyo. Hii si mara moja watu kuingia mkenge inapotokea wanakutana na hali hiyo.
Lazima uelewe serikali ya mwili wako inakutegemea wewe, ukiipeleka vibaya lawama zitakuwa juu yako.Usiwe na papara ya kutoa uamuzi wa kukubali uambiwavyo unapendwa bila kufikiria kwa kina.
Hakuna hata siku moja mtu anayekutaka kimapenzi akuambie anakuchukia. Fikiri kabla ya kutenda na kuona kauli uliyopewa ina nia gani na wewe, kweli anakupenda au anataka kukuchezea na kukuacha.
Katika uchunguzi wangu nimegundua wengi hupima kwa masikio juu ya kile aambiwacho na si kufikiria nini hasa kilichomvutia aliyekutamkia maneno hayo.
Japo kakutamkia anakupenda, ni vema ukafanya kadiri uwezavyo kupata muda kufikiria kwa kina kabla ya kutoa uamuzi wowote ambao unaweza kukufanya uwe na faida au hasara... Tutaendelea
Sign up here with your email