Na Ndaya Mgoyo, Mwananchi
Kwa ufupi
- Mama yake mzazi aliamini kuwa mtoto huyu ni mkosi asiyestahili kulala ndani ya paa la familia. Alimwona sawa na wanyama aliowafuga ndiyo sababu akamweka nao katika banda moja kwa miaka 10
Akiwa katika shughuli zake za nyumbani, mara akatokea mtoto mdogo wa jirani yake aitwaye Jane.
Binti huyo akaanza kucheza na wenzake kwa dakika kadhaa na mara akaacha michezo na kuanza kukimbia kuelekea nyumbani kwao.
Wenzake wakamuuliza “mbona unakimbia wakati bado
tunacheza”. Akajibu, “nakwenda kwenye banda la mifugo kumpa chakula Ben.
Muda umekimbia na hakuna mtu nyumbani”.
Kwa kauli hiyo, mwanamke huyo alitaka kujua iwapo
Ben anaishi kwenye nyumba ya jirani yake kwani ni miaka 10 imepita tangu
amtie machoni.
“Ben yupo na anaishi kwenye banda la mifugo. Huwa
anahudumiwa na mama, lakini kwa sasa mama hayupo na baba amekwenda
kazini. Mimi nina jukumu la kumpa chakula,” alijibu Jane.
Mama huyo akapata shauku ya kumtembelea mtoto huyo
kuona kinachoendelea kwa jirani zake, Lo! anachokiona haamini macho
yake; Mtoto Ben amefungwa kwa kamba kwenye kigodoro chembamba akiwa
hajiwezi kwa njaa.
Hivyo ndivyo alivyoibuliwa mtoto Ben baada ya kukaa katika banda la mbuzi kwa muda wa miaka 10 bila majirani kufahamu.
Ben, ambaye kwa sasa ana miaka miaka 14
alizaliwa akiwa kiziwi, bubu na ulemavu. Aibu ya kuzaa mtoto kama huyo
ndiyo ilifanya wazazi wake wamfungie kwenye zizi la wanyama kwa muda wa
miaka 10 na wakihakikisha hakuna jirani wala ndugu wa karibu
anayefahamu juu ya tukio hilo.
Historia ya mtoto huyo
Kwa mujibu wa baba mlezi Mr Jeremiah Mbusia,
ambaye ni askari katika Wizara ya Mali Asili, Narok Kenya, mtoto huyo
siyo wake wa kuzaa bali alifika katika nyumba hiyo miaka 12 iliyopita
akiwa na mama yake wakati huo mtoto huyo alikuwa na miaka minne.
Alilelewa katika nyumba hiyo kwa miaka miwili na
ndipo wazazi wake, yaani baba yake wa kambo na mama yake mzazi wakaamua
kumuweka katika kibanda kidogo nje ya nyumba yao na hutumiwa kama zizi
la mbuzi na kondoo.
credit mwananchi
credit mwananchi
Sign up here with your email