WANAFUNZI WAANDAMANA HADI KWA MKUU WA MKOA KWA KUKOSA NAFASI KIDATO CHA TANO MKOANI MBEYA

WAHITIMU 39 wa kidato cha nne mwaka jana katika Shule 
ya Sekondari Karobe jijini hapa wakiwa na wazazi wao, jana 
waliandamana hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa ili kujua hatma
 yao baada Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushindwa
 kuwapangia nafasi za kujiunga kidato cha tano licha ya 
kufanya vizuri katika mitihani yao.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanafunzi hao pamoja
 na wazazi wao, walisema kuwa waliamua kufika ofisi za 
Mkuu wa Mkoa ili kujua hatima yake, baada ya kuona hawapewi
 majibu ya kuridhisha kutoka kwa viongozi wa chini yake.


Walisema tangu wizara itangaze majina kwa ajili ya kujiunga
 kidato cha tano wiki mbili zilizopita, wameshangazwa kuona
 wanafunzi kutoka shule hiyo hawajapangiwa kwa ajili ya 
kuendelea na masomo katika ngazi hiyo, licha ya kuwa na
 ufaulu mzuri.


Wanafunzi hao ambao wamepata alama za daraja la kwanza
 hadi tatu, hawajui hatima yao kutokana na wizara husika
 kushindwa kuwapangia shule kwa ajili ya kuendelea na
 masomo ya kidato cha tano.
Nao wazazi ambao waliambatana na watoto wao hadi ofisi 
ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na Mbunge wa
 Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (CHADEMA) kwa nia ya
 kutafuta suluhu ya suala hilo, walisema kuwa tangu Wizara
 ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutangaza majina ya wanafunzi
 waliofaulu kwa ajili ya kidato cha tano na shule walizopangiwa,
 hakuna majina ya watoto wao.


Mmoja wa wazazi hao, Lawrance Shimo, alisema baada ya kufuatilia

 kwa kina ikiwemo kuuliza uongozi wa shule, walibaini kuwa katika 
shule hiyo hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyepangiwa shule kwa
 ajili ya kuendelea na kidato cha tano, licha ya kuwa na ufaulu wa 
alama mzuri
Previous
Next Post »

Blogger templates