MZEE WA MICHEPUKO KIBONDE, GADNA HABASH WAPANDISHWA KIZIMBANI LEO CHEKI PICHA HAPA....!!!

MTANGAZAJI wa Clouds FM, Ephraim Kibonde na mwenzake, Gadna Habash wa Times FM leo wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kusababisha ajali na kutoa lugha ya matusi.

Watangazaji hao wamesomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Salim Mohammed mbele ya Hakimu Aniseta Wambura.
Kibonde na Gadna wanadaiwa kutenda makosa hayo Jumamosi ya Agosti 9, mwaka huu saa 12 asubuhi, katika eneo la Makumbusho, ambapo Kibonde akiwa anaendesha gari walilokuwa wamepanda aliligonga gari la raia mmoja wa kigeni (Mzungu) na kukimbia.
Kesi yao imeahirishwa mpaka Septemba 10 mwaka huu itakaposikilizwa tena
Previous
Next Post »

Blogger templates