Mimi ni mwanafunzi wa chuo fulani hapa mjini, nilipata boyfriend nikiwa mwaka wa pili chuoni, alijifanya kunipenda sana hata kunirubuni nitoke hostel nikaishi nae kwake yeye alikuwa mwaka wa tatu ila alidai kuwa amepanga chumba mitaa ya sinza,. Nilikaa nae kwa muda wa miezi miwili kumbe kile chumba hakikuwa chake kilikuwa ni chumba cha kaka yake aliyekuwa amesafiri, aliporudi alinikuta mimi pale ndani nikiwa naishi na mdogo wake alishangazwa sana na kitendo kile cha mdogo wake. Jamaa alitufukuza wote kama mbwa na sasa hivi naishi tu kwa rafiki yangu kwani nimeshindwa kurudi tena hata hostel, kwani pesa niliyopewa kulipia hostel nilimpa boyfriend wangu huyo ili tununulie vitu vya kula ndani. daah iliniuma sana. Simuamini tena
Sign up here with your email