WATATU WAKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI MBAGALA, DAR

Ngozi ya chui na nyara nyingine zilizokamatwa.
Meno ya tembo yaliyopatikana kwa watuhumiwa.
Kamishna  Kova akionyesha baadhi ya nyara walizozikamata.
WANAWAKE watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi  kwa tuhuma  za kujihusisha na mtandao haramu wa nyara za serikali.  Watu hao walikamatwa  Julai 23 mwaka huu huko Mbagala-Mission jijini Dar es Salaam  baada ya jeshi hilo kupata taarifa kutoka kwa msamaria mwema kuwa eneo hilo kuna watu wanafanya  biashara hiyo.
Watuhumiwa hao ni Wamael Mshana, Upendo Mshana na Stella Daniel waliokutwa na pembe za ndovu zenye thamani ya sh. 49,750,000.Jeshi hilo pia linamshikilia Venance Manyikawa Mbagala- Mission baada ya kukutwa na ngozi ya chui kinyume cha sheria
Previous
Next Post »

Blogger templates