PICHA 2:MGOMBEA UBUNGE CHALINZE KUPITIA CHAMA CHA AFP AJERUHIWA KWA MAPANGA

 Mgombea Ubunge katika Jimbo la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Ramadhani Mgaya kupitia chama cha AFP amejeruhiwa kwa mapanga na watu wasio julikana. Mgaya amesema amevamiwa na kujeruhiwa na mtu ambaye hamfahamu majira ya saa sita za usku akiwa katika nyumba ya kufikia wageni ya Goodtime Chalinze.
 "Nimevamiwa na kujeruhiwa na mtu ambaye simfahamu ahsante uongozi wa chadema kwa kunisaidia,"alisema Mgaya.
Mgaya amesema ameumia mikononi wakati nikipangua nakujitetea mvamizi alikuwa na panga. Mbali na yeye pia amesema pia kiongozi wa Chadema, Mwita Waitara naealijeruhiwa kwakuwa alikuwa moja ya watu waliokuwa wakimsaidia. 
Father Kidevu Blog
Previous
Next Post »

Blogger templates