Bwana wa Wastara Adaiwa Kumpa Mimba Muhudumu wa Baa

Na Gladness Mallya na Hamida Hassan
MSANII wa filamu za Kibongo ambaye ni Mtangazaji wa Channel Ten, Bond Bin Sinan, anadaiwa kumpa mimba mhudumu wa baa maarufu ya Break Point (BP) iliyopo Kijitonyama, Dar, anayejulikana kwa jina moja la Grace (pichani).
Akizungumza na gazeti hili kwa huzuni kubwa, Grace alisema yeye na Bond ambaye kwa sasa anadaiwa ni bwana wa mwigizaji Wastara Juma, walikutana maeneo ya Masaki, Dar, Februari, mwaka huu ambako alikuwa akifanyia kazi awali na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi.
Alisimulia kuwa, katika kipindi hicho walikuwa kwenye mahaba niue ambapo mara nyingi alikuwa akitoka kazini anamfuata nyumbani kwake Mwananyamala, Dar.Aliendelea kufunguka kwamba alipomwambia tu kuwa ana ujauzito wake ndipo mambo yalibadilika huku jamaa akitibuka utadhani kamwagiwa pilipili iliyosagwa.
“Ukweli mwazoni mapenzi yalikuwa shatashata lakini baada ya ujauzito, jamaa aliniruka futi mia.
“Mwanzoni alitaka nikatoe lakini nikakataa na kumwambia kwa nini niue kiumbe kisicho na hatia ndipo akaingia mitini mpaka leo na ujauzito una miezi sita.
“Kila nikimwambia anasema siyo wake, ananitukana na mwisho aliniambia kwamba nisubiri mtoto azaliwe ndiyo tukapime DNA (vinasaba), sasa nateseka kuulea ujauzito peke yangu.“Naendelea kulea hii mimba, najua Mungu atanisaidia, nitajifungua salama na mwanangu nitamlea lakini inaniuma sana kutokana na majibu anayonipa na matusi ya kila wakati.
“Nimefikia hatua hii ya kuzungumza ili walau mnisaidie jamani maana naona ananisumbua na hanielewi.“Kuna siku nilikutana na aliyekuwa mpenzi wake (Anti Lulu), nikamwambia kila kitu akaahidi kunisaidia,” alisema Grace akimwaga chozi.
BOND ANASEMAJE?
Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilimsaka Bond na kummwagia kila kitu ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Huyo dada mimi simfahamu na ninaona wamepanga kunichafua yeye na Anti Lulu kwa sababu nina meseji nyingi sana za huyo dada, nimewasiliana naye Facebook akisema yupo naye hapo kazini kwake hivyo naomba mpotezee hizo habari siyo za kweli.”
Gazeti hili lilifanikiwa kuziona meseji za Bond alizokuwa akiwasiliana na Grace katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp ambazo zilikuwa zimejaa matusi yasiyoandikika gazetini huku akimtaka mwanadada huyo kusubiri ajifungue ndipo wakapime DNA ili kujua ukweli.
GPL
Previous
Next Post »

Blogger templates