Cristiano
Ronaldo ameendelea kumfunika mpinzani wake Lionel Messi, baada ya
kumshinda kwenye uchezaji bora wa dunia, ufungaji bora wa La Liga na
Champions League, na utajiri, sasa kwa mujibu wa taasisi ya uchunguzi na
uchambuzi wa masoko ya Repucom umemtaja mshambuliaji huyo wa Real Madrid kuwa ndio staa wa soka mwenye thamani kubwa kwenye masuala ya kibiashara.
Kwa mujibu wa Repucom
ndio mwanasoka mwenye mvuto mkubwa wa kibiashara kwa makampuni makubwa
duniani kutokana ufuasi mkubwa wa mashabiki alionao kupitia mitandao ya
kijamii.
Ronaldo ana likes millioni 82 kwenye mtandao wa Facebook, wakati
anayemfuatia Messi ana likes millioni 57, kwenye twitter Ronaldo tena
ameongoza kwa kuwa na wafuasi millioni 26.
Utafiti pia umeonyesha Ronaldo anatambulika zaidi duniani kuliko
wachezaji wenzie, akipata asilimia 87% ya watu waliofanyiwa utafiti huo.
Wachezaji wengine waliongia kwenye listi hiyo ya wachezaji wenye mvuto mkubwa wa kibiashara kulingana na umaarufu ni Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Gerard Pique, Fernando Torres, Wayne Rooney – hawa ndio waliounda Top 5
Sign up here with your email