Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Mstaafu Issa Machibya ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya maafa ya Mkoa amesema kuwa bado idadi maiti zilipo kwenye maji ni kubwa ambazo bado hazijapatikana.
''Zoezi hili linakuwa gumu sababu ya uhaba wa waokoaji pamoja na miundombinu duni ni kikwazo katika zoezi hili la ukoaji lakini bado tunaendelea na kazi ''alisema Mkuu wa MkoaWanajeshi wa jeshi la wananchi (JWTZ) wakiendelea na zoezi la kuopoa miili ya watu waliopata ajali ya mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo baada ya mitumbwi waliyokuwa wakisafiria kuzama. Waokoaji wakiwa wamebeba mwili uliopatikana katika ziwa Tanganyika baada ya ajali ya mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo.Zoezi la uopoaji wa miili linaendelea na vikosi mbalimbali vya ukoaji katika ziwa Tanganyika kufuatia ajali ya mitumbwi iliyotokea jana.
Viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakiwa katika eneo la ajali wakiangalia zoezi la upoaji wa miili iliyopatikana katika ziwa Tanganyika kufuatia ajali ya mitumbwi iliyotokea jana mchana kutoka kushoto ni Amani Kaburu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa kigoma anayefuata ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya anayefuata ni Katibu Tawala wa Mkoa John Nduguru na Ramadhani Maneno Mkuu wa Wilaya ya Kigoma.
Sign up here with your email